Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact



(Words of the Spirit)

Maneno ya Roho

MANENO YA UNABII, MANENO YA HEKIMA, UFAHAMU, NA MAARIFA WAKATI

ULIOPITA, ULIOPO NA UJAO


Note: The following prophetic word have been translated from English to Swahili. We have not changed them, adulterated them or doctored them up. Scriptures have been added to some subtitles in order to draw the readers attention to their content.

 

TATIZO NI HILI. (THE PROBLEM IS THIS.)

“...The problem is this, and it has always been this: man will not let me have the preeminence...”. Our Sustaining Bread Vol.4 Issue 6, pg 22


Tatizo ni hili; na mara zote limekuwa hili: mtu hamruhusu Mungu amtawale kikamilifu. Lakini Mungu ampatapo mwanaume, wakati ampatapo mwanamke ambaye atajinyenyekeza mwenyewe na kumruhusu Yeye ayatawale maisha yake kikamilifu, Mungu hatakuwa na mipaka katika kutembea, kwa maana anapenda kutembea, na anapenda kuonyesha utukufu wake, na anapenda kuionyesha nguvu yake. Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.(Eze.22:30). Lakini watu wanamwonea aibu Mungu na wanamsumbua na wanamfungia nje. Wanamfungia kwenye boksi na kumwekea mipaka. Lakini wakati wanadamu watakapo jiachilia wenyewe kwake, Mungu atatembea. Atatembea kwa ajili yako, kama utajiachilia mwenyewe kwake, kama utamruhusu Yeye kushikilia lijamu, kama utamruhusu Yeye akumiliki kikamilifu, kama utamruhusu Yeye awe jinsi alivyo, utaiona nguvu yake ikifunuliwa katika njia nyingi za utukufu, kwa maana Mungu anatamani kutembea.


Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni (Mt. 7:21). Wapo wengi wasemao kuwa ni wa Kristo, lakini hawaendelei kwa bidii katika kazi Yesu aliyowapa, lakini watajitafutia njia yao wenyewe, miliki yao wenyewe na hawatatafuta kuendeleza Ufalme wa Mungu. Wachache sana ni wale ambao watatenda kazi kwa Mungu kikamilifu na kuendelea. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.(Ufu.2:10).Uwe miongoni mwa wale watakaoendelea na hawataanguka njiani, lakini wale watakaotii hadi mwisho. Ni wachache na ni mbali sana kati ya wale watakaoendelea katika kazi aliyoitoa Bwana na Bwana kupokea utukufu kama ambavyo angetoa.


Watu wengi hujinenepea na kuridhika katika maisha haya, na wanasahau kuhusu watu wengine, na wanasahau kwamba watu wanapotea katika dhambi. Wanajijengea ufalme wao mdogo, na kujipongeza kwa makofi mgongoni na mfumo wao wa usalama, na kudhania wanampendeza sana Mungu. Usitafute kujitosheleza wewe mwenyewe, usitafute dhawabu yako mwenyewe, lakini tafuta badala yake kwamba Yesu akaweze kutukuzwa, kwamba akaweze kutangazwa kwa wale wanaopotea.


Yesu ni Mungu wa viwango. Kuna viwango ambavyo huwaitia wanafunzi wake. Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu (1 Pet.2:9).


Watu wote walimaanishwa kuwa ukuhani wa kifalme na kuwa uzao mteule lakini watu wamebadili kweli ile na wameifanya kwamba ni wale waongo wanaolipwa tu ndio ukuhani wa kifalme, na wengine wote wanaruhusiwa kufanya kile wanachotaka kufanya, kufanya kitu chao wenyewe. Lakini huo ni mtego wa uwongo wa kunasa roho za watu. Imekuwa ni shauku ya Mungu kushirikiana na watu wake, lakini kwa sababu watu wake wamejitenga naye, wanatembea katika kuchanganyikiwa, lakini sio shauku ya Mungu watu wake wangechanganyikiwa, lakini wakati wanapojaribu kunywa katika chemichemi mbili wakachanganyikiwa. Mtu hawezi kunywa katika chemichemu ya uzima na chemichemu ya kifo na kubaki safi, bali atachanganyikiwa na atakuwa mjinga.


FALME MBILI (TWO KINGDOMS)

“...I say you are living in times when men have been taught that they may stradle the fence and live in two kingdoms....” Our Sustaining Bread Vol.2 Issue 1, pg.20-21


Huwezi kuishi katika falme mbili. Watu wamefundisha kila aina ya uwongo kudhoofisha neno la Mungu, kudhoofisha kile Kristo alichosema, kudhoofisha kweli yake, wakaanzisha desturi zao. Ni wadhaifu kwa sababu wanajaribu kuishi katika falme mbili. Huwezi kuishi katika falme mbili. Kama umezaliwa mara ya pili, unatakiwa kuishi katika ufalme wa Mungu. Mungu kama baba mwenye uchungu na watoto wake, Bwana Mungu aliye Hai amezaa watoto wengi juu ya nchi, lakini watoto wake wamepotea mbali na Yeye. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. (Mt.6:33).

 

KUSANYIKO LA KABILA LA ROHO. (GATHERING OF GOD’S SPIRIT TRIBE)

“...I am a father well grieved and in many sorrows for the actions of my children...” WOS. Issue 5, Radio Message # 56, pg.27


Wengi wamekufa, wengi wamepotea ingawaje aliwapa uzima, kwa maana waliukanyaga uzima na wala hawakuutunza. Waliutapanya na wakajiwekea urithi kama mwana mpotevu. Hawakurejea. Yeye ni baba mwenye uchungu kwa maana amewatuma manabii wake, amewatuma watumishi wake, amewatumia neno lake akiwaita watoto wamrudie, lakini wamemkataa kabisa. Wakapanga hata kuwaharibu watumishi waliotumwa kwao, na ni watoto wasiojali, walevi, waendao katika njia zao wenyewe. “.....kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea naye amepatikana. (Mt.15:24). Ni watoto waliojaa unafiki, watoto waliojaa uongo, watoto waliotengana na Mungu. Yeye ni baba mwenye uchungu sana na katika huzuni nyingi kwa ajili ya matendo ya watoto wake. Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akapangisha wakulima, akaenda akakaa katika nchi nyingine muda mrefu. Wakati wa mavuno alituma mtumwa kwa wale wakulima ili wampe baadhi ya matunda ya mizabibu; wakulima wakamfukuza na kumrudisha mikono mitupu.....Atakuja na kuwaangamiza wakulima wale, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.(Mt. 20:9-10, 16). Lakini muda umewadia, na hataona uchungu tena, na wala hatahuzunika tena kwa maana atawakataa watoto hao na atawaacha katika ukorofi wao na atawaleta wale ambao hawajasikia neno lake. Atawaleta watu wa roho ambao watamtii yeye katika roho na kweli. Atawaleta watu mbali na wale wanaojulikana kwa jina lake.


Yeye ni baba aliyepatwa na uchungu kwa muda mrefu mno, na sasa atainua na ataondoka kwa wale walioondoka kwake na kumwacha. Ataacha wakiwa wamekataliwa. Atawaacha ukiwa. Naye atawaleta watoto wapya, watu ambao hawakumjua Yeye, wala kuliitia jina lake. Ataituma Roho yake juu yao nao watamjia. Watamshiriki Yeye nao watafurahi kwa fursa ya kuwa watoto wake, nao watafurahi katika Yeye nao watatii. Hawaja asi juu yake, lakini wamengojea kwa kiu na njaa na sasa ataituma Roho yake nao watakusanywa hata mwisho wa dunia.Watakusanyika kwake naye atakuwa Mungu wao nao watakuwa wanae.


Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao. (Mt.8:22). Atawaleta watu wake watakatifu, nao watafurahi siku zote kwamba yeye ni Mungu wao, nao wataimba nyimbo za Sayuni kwake. Ataongea nao nao watasikia haraka nao watapiga magoti na kumpigia magoti kwa sababu mioyo yao atafurika kwa upendo wake. Atawaacha wafu wazike wafu wao wenyewe na walio hai watachanua uzima katika Yeye. Atawainua watu ambao watakuwa na neno lake katika midomo yao na litakuwa ni neno lililo hai.


SIO KITU KIGUMU. (IT’S NOT COMPLICATED)

“... it is not a difficult thing to follow after me. But I say that men bring about the difficult by their crafty inventions...”. WOS Issue 32, pg.1


Sio vigumu kumfuata Mungu, lakini watu huleta ugumu kwa uvumbuzi wao wa hila, wale wawazao ndoto, wafikirio mifumo, wafikirio hila za kufanya iwe ngumu kumfuata Mungu. Wanaleta kuchanganyikiwa, wanaleta upotofu, wanaleta kila namna ya undanganyifu. Wanafanya hivyo kwa sababu wao wenyewe wanapenda kuwa Mungu, wanapenda kuwa wafalme kwenye kiti cha enzi. Wanaweka nadharia zao na mawazo yao, wanapanga uhila na uwongo. Wanawaleta watu katika vifungo, wanawaleta katika kuchanganyikiwa na upotofu. Ni nani aliye na hekima, naye ayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za Bwana zimenyooka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake. (Hos. 14:9). Lakini njia ya Mungu ni safi, ni rahisi na haijanajisiwa. Sio ngumu, haina mambo mengi, lakini ni halisi.Wale waingiao katika kuchanganyikiwa, huingia kwa ajili ya kujiangamiza wao wenyewe.

 

KUJIFUNZA SIKU ZOTE. (EVERLEARNING)

“....do not seek to be everlearning yet never coming to a knowledge of truth....”. WOS Issue 32, pg.1


Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kufikia ujuzi wa kweli. (2 Tim.3:7). Usitafute kujifunza sikuzote, na bado usiweze kabisa kabisa kufikia ujuzi wa kweli. Wako watu wengi walionaswa katika mtego huo kwa sababu hawamtafuti Mungu. Wanatafuta maarifa ambayo yatawafanya waonekane kuwa na maarifa zaidi ya mtu aliye mbele yake.Mara zote lengo lao ni kiburi, na ukorofi, nia yao ni kujipenda wenyewe na kujiabudu. Sio Mungu wamtafutaye kumjua, hapana kabisa. Kwa maana yeyote atakaye kumjua Mungu, Mungu atajifunua kwake. Ambaye anatafuta maarifa kwa ajili ya maarifa anatafuta kuchanganyikiwa.


Anatafuta kile kitakachomfanya aonekane yuko juu kuliko ndugu yake. Ukweli wa jinsi Mungu alivyo unapatikana kirahisi na kwa kumwamini Yeye. Bwana Yesu hajawaita kujifunza siku zote, ila msiweze kabisa kufikia ujuzi wa kweli. Bwana amewaita kumjua Yeye kwa maana ni Mungu wenu. Utamjua Yeye utakaponyenyekea mara zote mbele zake na kumwamini na kumtegemea. Utamjua utakapomruhusu akupime na akujaribu na utatoka ukiwa msafi. Lakini kama utajifungia mwenyewe kwenye kitabu, baada ya kitabu, ukitafuta kujifunza siku zote, unajipeleka mwenyewe kwenye kuchanganyikiwa.


UJUZI HULETA MAJIVUNO. (KNOWLEDGE PUFFS UP)

“...I am gained by being yielded over in the Spirit, for it is the Spirit that gives thee life...”. WOS Issue 32, pg.2


Mungu hapatikani kwa ujuzi kwa maana ujuzi huleta majivuno. .....Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. ( I Kor 8:1). Mungu anapatikana kwa kujiweka chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu kwa maana Roho ndiye atoaye uzima.......kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. (2Kor.3:6). Ni Roho wake Mtakatifu atakayewaongoza na kuwatia katika kweli yote. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote;..... (Yn.16:13). Katika saa hii katika kizazi hiki, kuna wengi wawezao kuona kosa, dosari, matatizo, lakini wenyewe wala sio afadhali. Wakati macho yao yamefunuliwa kuona hayo yote, bado hawatembei na Mungu. Wanaangalia tu kanisa na kuchunguza, wanachunguza, wanachunguza kila kosa, lakini hawaitafuti njia ya haki.Wako wasio na idadi waliotoka nje ya mfumo wa kidini, lakini hawatakwenda kwenye kusudi la Mungu. Wanapenda tu kukaa na kupika majungu, kusengenya, kula na kutafuna mzoga ule waliouacha.

 

Kiuhalisia hawajatoka huko, ingawaje uwepo wao wa kimwili umeondoka. Bado wako kule katika mioyo yao na katika nafsi zao. Bado wako kule katika matakwa yao, kwa maana hawajataka kujitenga kikamilifu, badala yake wanabakia katika mawazo yao, katika maneno yao, katika matakwa yao, wamebakia. Kwa hiyo hao sio wanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo kwa maana hawaji kwake na kulitafuta kusudi lake. Kama mtu hayuko kwenye kusudi la Mungu, hana maana yeyote. Lakini mtu anapokuwa katika kusudi la Mungu, ndipo anapoongozwa mbele, ndipo anapopewa kweli, ndipo anapopewa nuru.


MAFUNDISHO YA MASHETANI. (DOCTRINES OF DEVILS)

“...I never call my people to be enticed by seducing spirits and doctrines of devils...”. Bread for the Nations. Issue 30, Radio Message # 1529, pg.17


Mungu hajawaita watu wake wategwe na roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Watu wengi katika saa hii wamejiweka wenyewe kwenye mafundisho ya mashetani na hadithi zidanganyazo kwa sababu ya kutoshughulikia tamaa za mwili. Kwa sababu wanafanya hivyo, wanakuwa rahisi kuwindwa na mafundisho ya mashetani na roho zidanganyazo. Basi Roho anena wazi wazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho nzidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; (I Tim.4:1)


Wakati watu wanapoachia mwili kutawala,wanakuwa rahisi kumezwa. Adui anachezea kile ambacho ni cha mwili katika mwanadamu, na ambacho ni mnyama. Wakati mtu hajilindi dhidi ya tamaa katika mwili wake mwenyewe, anaweza kukumbwa na roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Wako wengi katika kizazi hiki wanaohubiri kwamba utajiri ni ishara ya fadhila za Mungu kwao. Wanahubiri kwamba kwa wingi wa vitu vya dunia hii mtu alivyo navyo, ndivyo Bwana Mungu alivyompa fadhila. Kwa kweli hayo ni mafundisho ya shetani na zinawadanganya watu wa Mungu katika maana halisi ya msalaba. Wanawapeleka watu wa Mungu kwenye kile ambacho ni ukahaba, kile ambacho ni uzinzi, kile ambacho ni utupu.


KANISA LA KWANZA. (THE FIRST CHURCH)

“....every one says “the first church, the first church, the first church” I say every one says, “let’s return to the book of Acts” but no one will give up their lives...”. Thus Saith the Lord. Bread for the Nations Issue # 40 pg. 4


Kila mtu anasema, kanisa la kwanza, kanisa la kwanza, kanisa la kwanza Kila mtu anasema, “na turejee katila kitabu cha Matendo ya Mitume lakini hakuna hata mmoja atakaye yatoa maisha yake. Wale waliotembea na Kristo mwanzoni waliyatoa maisha yao. Ni kwamba hawakulinda haki zao katika maisha, hawakutafuta kuishi katika starehe na anasa na wala kukubaliwa na watu. Mioyo yao ilijikita kwenye kusudi moja ambalo liliwasukuma hadi kifo. Mungu anawapenda watu wenye kiu na njaa ya haki yake. Hawapendi watu wenye kiu na njaa ya vitu vya dunia hii, vitu ambavyo vitapita. Anatamani watu watakaojitoa kwake kikamilifu, kwa furaha, kwa kutoa shukrani na sifa. Kwa maana uitikiapo wito wa kiroho, kwa kuwa Mungu ni Roho atakuongoza ipasavyo.


Roho ya Bwana i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta, niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. (Isa.61:1).


Kwa maana katika kizazi hiki anainua wale watakaomkabidhi maisha yao wakaweze kuongozwa na Roho Mtakatifu, kutolewa nje ya magereza, kuweweka mateka huru, kuongozwa nje ya vifungo na kuwaweka mateka huru. Kwa maana kuna mamilioni waliopo utumwani, utumwani katika giza, katika uovu, katika kifo, Mungu atatuma mashahidi wake, jeshi lake la Roho duniani kote, nao watakuwa tangazo la Mungu la kweli,tangazo la jinsi alivyo, watakuwa kama hao wafunguao wafungwa,wao wawekao huru walio katika vifungo na ukandamizi mkali.


Mkutano mkubwa, mkutano mkubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana i karibu, katika bonde la kukata maneno. (Yoeli 3:14). Kwa maana wako watu wengi sana katika bonde la maamuzi. Kuna watu wengi sana watapotea kama hawatapokea ukweli. Bwana Mungu aliye Hai atakuwezesha na atakutia nguvu na atakutuma kama sadaka kwa wengine na utaipata furaha yako katika kutumwa huko.


Ni Mungu aliye Hai atakaye kupa wewe changamoto ili kusimama katika Yeye. Ataenda kukupima na kukujaribu ili kuona kama utasimama katika kweli. Wala usimtafute yeyote wa kumshtaki au kulaumu lakini ujue kwamba ni Mungu aliye Hai aliwekalo hili mbele yako. Fahamu kwamba atakupima na kukujaribu, kuona kama unasimama katika kweli aitoayo. Hakuna njia nyingine ya kuingia katika ufalme wa Mungu mbali na njia aliyoitoa Bwana Yesu. Njia aliyoitoa ni mateso, ni udhia, ni aibu kwa ajili ya jina lake. Wakati unapokuwa tayari kubeba dharau kwa ajili yake Mungu aliye Hai, utaingia kwake.

 

Utafuteni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kutoa unabii. (1Kor. 14:1). Kama uko makini na Bwana Yesu, basi omba kwa ajili ya moto wake mtakatifu uje juu yako, ukuunguze, omba kwa moyo wako wote naye atakusikia. Tamani sana karama za rohoni, karama ambazo zitakupa wewe nguvu, zitakazokupa wewe utukufu, karama ambazo zitakuleta kwenye unyenyekevu, na katika nguvu za uwepo wake. Wale watakaomtii Mungu katika kizazi hiki watatiwa nguvu sana na Roho wake Mtakatifu. Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. (Kol. 3:1-2). Inampendeza Mungu sana kuwapa watu wake karama, naye anataka kama ungetamani sana karama za rohoni zaidi sana ukaweze kutoa unabii. Usitamani hazina za Sodoma, wala usiangalie mazuri ya misri, lakini tafuta vitu vya Roho wa Mungu ambavyo vitadumu.


Vitu vya rohoni vitakutia nguvu, na kukutajirisha na kukunyenyekeza na kukufanya umjue Mungu aliye Hai jinsi alivyo. Mungu anakuagiza kutamani hazina za rohoni. Hapendi ujipoteze mwenyewe kwa vitu vile vinavyopita. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vinatokana na dunia. (1Yoh 2:15-15).


WANA NA WATOTO WAMELISHWA TAKATAKA. (MY BABIES AND CHILDREN HAVE BEEN FED GARBAGE)

“....For too long, my babes and children have been starved, they have been deprived, they have been fed garbage....I say I have had enough...” WOS Issue 12. Radio Message # 137 pg.18


Kwa maana ni siku nyingi, wana wa Mungu, watoto wa Mungu wamelishwa takataka, wamekuwa wakipewa mabaki ya dunia hii, wamekuwa wakilishwa uchafu wa Sodoma, uovu wa Gomara na machukizo ya Misri, na Mungu amevumilia ya kutosha. Usiwe miongoni mwao walishao sumu watoto wa Mungu. Kweli Bwana Mungu anatamani mngekuwa kama kina mama wanyonyeshao, wakiwa wamewabeba watoto, wakiwapa chakula cha kweli cha uzima wake, Neno lake, akiwapa chakula cha kweli kidumucho, ambacho ni cha milele.


Usiwe na damu za watu wasiohesabika mikononi mwako ambao hawajapokea hata chembe ya utukufu wa Mungu, ambao hawajapokea hata chembe ya utukufu wa Mungu, ambao hawajapokea hata chembe ya nguvu za Mungu, ambao hawajapokea neema ya damu yake ya ukombozi. Yeye ni Mungu mtakatifu, naye huwapa hazina zake za kiroho wale wazitamanio sana karama za rohoni.


UDHIA NA MATESO. (PERSECUTION AND SUFFERING)

“....I the Living God have promised the persecution to all of those who will live godly in me...”. Our Sustaining Bread Vo. 4 Issue 7, pg.38


Bwana Mungu ameahidi udhia kwa wale wote watakaoishi maisha ya utakatifu katika Yeye. Kwa hiyo kama ukiudhiwa kwa ajili ya jina lake, furahi, furahi na ufurahie. Kwa maana ni bahati sana kuudhiwa kwa ajili ya Bwana Yesu. Hii inathibitisha kuwa wewe ni tishio kwa adui, hiyo inathibitisha kuwa unatembea pamoja naye, hiyo inathibitisha kuwa unaweza ukafurahia. Naam , na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. (2Tim.3:12). Watu wengi wapo kuzimu hata sasa kwa sababu walikua kistarehe. Walidhani haifurahishi kwao kujikita kwa Bwana Yesu, wakachagua njia ya usalama, njia ya starehe, njia isiyo na vita na hivyo kupoteza nafsi zao. Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. (Yn. 17:14) .


Mungu amewaita watu wake katika udhia, mateso yajayo kwa kule kufananishwa naye. Mungu amewaita watu wake kukosa starehe, kukosa raha katika miili kwa wote wale watakaomfuata Yeye kikweli. Usalama wako haupo katika kitu chochote kilichopo duniani. Usalama wako unapatikana katika kuyatoa maisha yako yote katika Kristo. Ukweli ni kwamba maisha yako sio yako kabisa kama unadai wewe ni mali ya Kristo. Acha maisha yako yakae mahali pake panapohusika ambapo ni katika mikono ya Mungu. Wala usidharau udhia, mateso, aibu na huzuni ambayo Yesu huiruhusu kwa yule mtu wake wa kweli kuipata ili akaweze kuwa kitu kimoja na Yeye. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakaye okoka. (Mt.24:13).Yesu alipitia maumivu kukuenda wewe, kadhalika nawe vumilia kwa ajili ya wengine, kwa sababu Yesu alivumilia kwa ajili yako. Usiangalie mambo yako mwenyewe bali mwangalie Kristo kwa sababu Yeye ni Mungu wao. Usiishi kichoyo, lakini ishi ukiyatoa maisha yako. Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. (2 Tim. 2:3)


JIBU. (THE ANSWER)

“...I say that no man knows the answer because the answer does not lie with men. But I say that the answer is to be found in serving me. Thus Saith the Lord...”. Issue # 39


Hakuna mtu awaye yote ajuaye jibu la kanisa kwa sababu jibu haliko kwa wanadamu. Jibu linapatikana kwa kumtumikia Mungu. Ni katika Bwana watu watahifadhiwa katika saa ya uovu, hiyo ni kwamba wakaweze kuongozwa katika nuru Yake, kuelekezwa na kuomgozwa naye.


Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. (Mt. 11:28). Wakati Bwana Mungu atoapo mwaliko kwa watu wake, ni kwamba watu hao waweze kumkimbilia na kuwa salama, ni ili kwamba watu hao waweze kukombolewa. Hatoi mwaliko kwa mwanamume au mwanamke ili kwamba wamkanyage, na kutafuta kumuasi Yeye siku zote.


Lakini anawaalika ili kumjia ili kwamba akaweze kuwafariji, na akaweze kuwapatia amani yake na usalama. Wakati mwanamume au mwanamke aitikiapo mwaliko huo na lakini wakatafuta kumuasi Yeye, kila siku wanakuwa chukizo kwake na huzuni kubwa. Wako wengi ambao wataangamizwa, lakini kuna masalia ambao watabakia, ambao watasikia wito wake na kumwendea nao watakuwa watu wa rohoni. Kwa maana ni siku nyingi mno Mungu amengojea watu ambao watamjua Yeye. Ametamani watu watakaokuwa wa kweli, watakaomtumikia na hakuwapata. Katika kizazi hiki na kizazi kijacho, kutakuwepo na wale watakaokuwa kweli, na watakuwa ni wale waliotoka kwenye uharibifu, nao watamjia na kumtumikia. Wakati watu wa Mungu ni wenye haki, wataondoka kwa viongozi waovu.


Kuna masalia na Mungu anaongea nawe vile vile, anakuita kwa sababu moyo wako u mwororo, na anakuita wewe kwa sababu unatamani kuwa safi, unatamani kuwa mtakatifu, anakuita wewe kwa sababu unatamani kumjia Yeye, na anasema leo hii, njooni kwangu ninyi nyote, njoo katika utukufu wake, na njoo katika nguvu zake. ‘.......watu walioharibika akili zao, waliokosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida’. (1Tim.6:5). Wengi wamenaswa kwa maana wapo watumishi wengi wa uwongo wafundishao kuwa utakatifu ni njia ya kupata faida. Watumishi kama hao, jiepusheni nao kwa maana ni watumishi wa uwongo na umrejee Mungu aliye Hai. Jifanye mwenyewe maskini kwa furaha. Ni afadhali uwe huna kitu kuliko kuwa na vitu vya kukuua.


Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? (Mk. 8:36). Kuna mafundisho katika kizazi hiki kwamba ni aibu kuwa maskini na kama wewe si tajiri, na kuongezewa vitu wewe sio wa ufalme wa Mungu lakini hata mafundisho hayo ni ya uwongo; kwa maana Mungu atawajali wale wapendao kujifanya maskini ili wakaweze kuwa matajiri katika yeye. Kuna wengi katika kizazi hiki watumiao kulazimisha kisaikolojia kwamba watu wajisikie hukumu kama hawatoi na kuwatishia. Lakini wanapowatishia, washurutisha na kuomba omba usiku kucha, wanajisikiahukumu na hivyo hawatoi.


UTOAJI. (GIVING)

“...I say look at the pattern and the example, not once do you see the principle of demanding and threatening and commanding in reference to supply, in reference to provision...”. WOS 1ssue 4, pg. 32-34


Angalia katika vielelezo na mifano, hakuna hata mara moja utaona kanuni ya kudai na kutishia na kulazimishia katika habari za utoaji au kupewa. Bali kitu kinapotolewa, kiwe kidogo kiasi gani, kinainuliwa juu na shukurani inatolewa, na kinazidishwa. Wale walio kwa kweli katika Kristo watajifunza kanuni hizo kwa maana yeye ni Mungu wa kuzidisha na anaweza sana kutupatia. Akasema, nileteeni hapa. Akawaagiza mkutano waketi katika majani;akatwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa mkutano. (Mt.14:18-19).


MUNGU ATAINUA MASALIA. (I SHALL RAISE UP A REMNANT)

“...I say though you live in a time when men’s hearts are hard and their eyes are turned towards evil, I say unto thee that in the midst of a rebellious generation that I shall raise up a remnant, I say I shall raise up a remnant of holy people who will obey me...” WOS Vol. 1 Issue 2 pg.7-8


Ingawaje mnaishi katika kizazi cha uasi, ingawaje mnaishi katika nyakati ambazo mioyo ya watu ni migumu, na macho yao yamegeuzwa kuelekea uovu, katika kizazi cha uasi Mungu atawainua masalia. Atawainua masalia ya watu watakatifu ambao watamtii Yeye, ambao watasema katika haki yake, ambao watafurahi kupokea. Atawainua na itakuwa ishara na maajabu kati ya kizazi cha uasi, kwa maana wakati watu wote wanaelekea katika kifo, atawaleta masalia ambao wanatamani uzima, na atafanya hivyo kama ishara na maajabu. Basi vivyo hivyo wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. (Rum.11:5). Mungu anaweza, kwa maana wakati watu watakapomjeukia Yeye kwa mioyo yao yote wajapopita katika bonde la uvuli wa mauti, hawataogopa mabaya kwa maana atakuwa pamoja nao. Mungu anainua masalia ambao hawatadanganywa, anainua watu wake wa Roho ambao watamjua Yeye jinsi alivyo. Watamtangaza Yeye na watamtangaza katika kweli. Watamtangaza jinsi alivyo kwa watu wengi. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wamauti, sitaogopa Mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. (Zab. 23:4)


Ni yeye Mungu aliye Hai ambaye atainua kati ya vizazi vilivyoko kutoka kwao watu watakaoamini katika Yeye. Itakuwa kweli ni hukumu dhidi yao kwa sababu wao wenyewe walikataa kuamini. Hebu tafakari kizazi cha kwanza kilichotoka Misri kiliangamia nyikani. Bado Mungu akachukua watoto wao nao na wakamwamini na kumtumaini Mungu. Ilikuwa ni yeye Mungu aliyewapa hazina ya nchi ya ahadi aliyowaandalia. Hivyo ndivyo kutoka kwenye viuno vya kizazi kisichoamini kwamba Mungu aliye Hai atawaleta watu ambao wataamini. Ambao ni watu watakaowaaibisha mababa zao watakaoangamia njiani. Wakati mwonapo watu katika giza kuu na katika upofu, watupieni kamba ya matumaini ili kwamba wakaweze kuja, lakini kama wakikataa tumaini, wala msiangukie gizani pamoja nao, bali endeleeni mbele kwa maana kutakuwepo na wale watakaonyoosha uchaguzi wao wenyewe, lakini watakuwepo wengine ambao wataletwa na kupewa matumaini na kujiimarisha. Watupieni kamba wale wanaozama, lakini kama wakikataa, usianguke pamoja nao bali endeleeni mbele katika Bwana.


BENDI YA MAPAMBANO. (THE MILITANT BAND)

“...I the Living God do put forth the call in this generation, .....I am calling forth my millitant band...,” Bread for the Nations Issue 14. Radio Message 162 pg. 19-20


Bwana Mungu aliye Hai anatoa wito wake katika kizazi hiki. Yeyote aliye na sikio la kusikia, sikia kile Mungu asemacho kwa maana anaita bendi yake ya mapambano. Hawatakuwa watu waliovalishwa silaha za kimwili, lakini watakuwa watu waliovishwa katika nguvu na utukufu. Watajua kuwa Yeye ni Mungu wao, muumbaji wao, asili yao, Mfalme wao. Nao watajua kama Yeye ni kamanda wao awaongozao katika vita ya utukufu. Mungu anatoa wito na wale watakaokuwa na sikio la kusikia, wale watakaomwitikia Yeye, hakutakuwa na nguvu au utukufu watakaonyimwa.


Mungu anainua bendi yake ya mapambano nao watakwenda hata mwisho wa nchi, wakimtangaza Yeye jinsi alivyo, wakimtangaza katika nguvu, wakimtangaza katika utukufu, wakimtangaza kwa ujasiri wote kwa maana watakuwa wameunguzwa na moto wake nao watakuwa wamewekwa lakiri kwake nao hawataona aibu kumtangaza Yeye. Kwa maana muda mrefu mno watu wameona aibu kumtangaza Mungu.


Kweli wakati watu watakaposimama wima na kutembea wima na kushika mahusiano sahihi na Mungu, wakati watakapotafuta kutii amri zake kwao, wakati watakapotafuta kumtumikia kwa miyo yao yote, hakuna nguvu atakayowanyima watu kama hao. Kweli watakuwa bendi yake ya mapambano, kwa maana wanapambana kwa ajili ya kweli. Wanapambana kwa ajili ya dhambi na uovu na upotofu na uharibifu. Kwa maana bendi yake ya mapambano itawaleta watu wanaofanana nao. Watawaleta watu wa moyo wa toba, wapendao kuunguzwa na moto, wapendao kusonga mbele, wapendao kumhubiri Yesu. Jiunge na bendi yake ya mapambano, Mungu atafungua milango ambayo mwanadamu hajawahi kuifungua, hawataamini kwa jinsi ambavyo hakuna mtu awezaye kutoa hivyo, naye ataonyesha bendi yake ya mapambano kuwa utukufu katika dunia hii.

 

KAMBI YA DAUDI. (DAVID COMPANY)

“...I am raising and Iam calling forth my David Company...”. Issue 14 Bread for the Nations Pg.22, & Bread for the Nations. Issue 16. pgs 25-26


Wako watu wengi walioinuka katika kizazi hiki, wako maadui wengi wa kweli ya Mungu na wako maadui wengi wa kusudi lake. Wanejiunga wenyewe kuwa jitu kubwa kama Goliati, lakini Mungu anainua na anaita kambi ya Daudi. Wataliua jitu hilo na hakuna kitu kitakachoendelea tena hapo. Watakuwa ni watu wasioona haya nao wataakisi utukufu wa Mungu, nao hawatakuwa na majivuno, kama wengi walivyo na majivuno, bali watakuwa watu wapole na wanyenyekevu. Watakuwa ni watu wenye sikio la kusikia, watakuwa ni watu wanaotafuta na kutamani kumwona Mungu. Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. (1Sam.17:45).


Wao ni wateule wa Mungu, ukuhani wa kifalme, Mungu aliye Hai atadhihirisha utukufu wake duniani, kwa maana wengi wanalia na kuomboleza wakimngojea Bwana, naye atakuja. Ataonyesha utukufu wake katika bendi yake ya mapambano. Goliati alijitanua mwenyewe na akajitangazia mwenyewe kuwa ni mshindi, lakini alikuwa mshindi dhidi ya jeshi ka kimwili. Alikuwa mshindi juu ya kile ambacho hakikuwa cha Roho wa Mungu, hakushinda katika roho kwa maana Mungu alituma kifaa chake cha Kiroho. Hakuna nguvu yake yeyote iliyoweza kushinda, na alikuwa ndiye Goliati aliyeangamizwa na kukosa matumaini. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme, na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. (Efe.6:12)


Mungu atainua Bendi yake ya kiroho katika kizazi hiki, nao watakwenda, nao watakuwa kama watu waelewao kwamba vita viko katika ulimwengu wa roho, na kushindana kwao si juu ya damu na nyama. Kwa maana saa ya Bwana imewadia, wale waijuae sauti Yake na kumsikiliza Yeye, watakuwa kama Daudi.Wataangusha majitu waliojiinua nao watafanya hivyo kwa silaha ya Bwana ya Roho wake. Askari wa Sauli walijipanga katika vita kuu na walizipanga silaha zao, lakini hawakuweza kushinda kabisa, bali walishindwa na kushindwa na kushindwa.


Goliati alijivuna mwenyewe kwa nguvu zake, utukufu wake na uwezo wake. Lakini Mungu alipotuna kifaa chake cha Roho, alishindwa kabisa na kuonekana hafai. Wala hakutawala tena kiushindi, bali alishindwa. Mungu ameinua Daudi wengi, amewainua watu wa Rohoni, nao watashinda, kwa maana Goliati hatatawala, lakini watu wa Mungu wa Roho walio katika kombania ya Daudi, watatawala.


 SHUHULI YA MSIMAMO MKALI. (AGGRESSIVE ACTIVITY)

“...you are meant to be engaged in aggressive activity for me...”. All Tribes Spirit Army Messenger, April 2010, pg.13


Ulimaanishwa kujiunga na shughuli za msimamo mkali kwa ajili ya Kristo. Ulitakiwa kutoa tamko kali la ufalme wa Mungu, tamko la rehema za Mungu na uzima. Mungu hakumaanisha watu wake wawe wapole,wawivu na wasiotaka kupiga vita. Ni kwamba ni lazima uyafukuze mapepo yanayokukalia, walioweka viota katika watu wako na wale uwapendao. Ni Bwana Mungu ambaye anatamani iwe hivyo. Kama ukikataa kupigana, basi ni rahisi kushindwa na kuchukuliwa. Kama ukitumia hayo Mungu aliyokupatia na kutimiza hamu ya Mungu kwako mapepo hayatashinda.


Kwa sababu wamekataa kuingia kwenye vita na kupambana katika vita iliyopo sasa, wamekataa kusimama kwa ajili ya Bwana, Mungu pekee na wa kweli na kuchukua aibu ipatikanayo kwake. Mlimaanishwa kuwa jeshi la wakombozi mliokombolewa. Kuna wengi katika kizazi hiki watetemekao nyuma ya mlango, wanaishi katika mtego wa hofu ambao Shetani amewawekea. Mungu atainua jeshi lake la wawekao huru, waliotiwa hamasa na Roho Mtakatifu, watakuwa watu watakaowatia wengine moto. Watatangaza kweli ya Mungu kwa ujasiri, na watakuwa tayari kuwaongoza mateka kwenye uhuru. Watawaweka wengi huru katika nyumba za vifungo vya hofu.


Wako wengi waliokula katika meza ambayo siyo. Wamekula katika meza ya uovu, na machukizo, na wamekula katika meza ya uchafu, na wamefanywa waoga. Bwana atawafanya kukaza nyonga zao na kujawa na nguvu zake, na kujawa na tumaini lake na utukufu wake. Kwa maana watu wake watakuwa waangavu, kama taa ziangazazo katika kizazi cha giza.


WITO WA WATU WA KIROHO. (CALLING FORTH A SPIRIT PEOPLE)

“...I am calling forth in this generation for a spirit people, for a people who will ascend in the dimensions wherein I dwell....”WOS. Issue 3, Radio Message #36, pg.42-46


Bwana Mungu aliye Hai anainua jeshi lake la kiroho, analileta jeshi lake la kiroho ambao watawakomboa walioko kwenye utumwa mkuu nao watakwenda mbele na upanga wa kweli.Utapenyeza giza nene na mwanga utadhihirika kwa wote watakaowaona waingiapo. Mungu anainua jeshi la watumishi,jeshi la ukombozi, ambao wataenda ulimwenguni kote, watatangaza kweli yake,watatangaza nuru yake, watamtangaza Yeye jinsi alivyo. Mungu anaita katika kizazi hiki watu wa rohoni, kwa maana watu watakaopaa mpaka kwenye mahali Yeye alipo, watu ambao watavuka mipaka ya kiwango cha kimwili na kuja kwake, katika ulimwengu wa roho.


Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. (Mt. 6:9-10). Hiki ni kizazi ambacho anatoa wito wake kwa ajili ya ufalme wake uje duniani, kama ilivyo mbinguni. Ameandaa safina ya rehema kwa wale wote wamjiao Yeye, ni ili kwamba mkaweze kuja kwenye safina ya rehema, kwa maana Yeye ni mwenye rehema.

Atakuinua wewe juu ya kiwango cha wanadamu na atakuleta katika kiwango cha malaika kwa maana anatamani mahali alipo na watu wake wakae hapo, kwamba mkaweze kuingia kwenye uwepo wake, na kuufahamu utukufu wake. Upendo wake ni kama mto usio na mwisho ambao utamiminika na wengi watakuja katika mto huo na kufahamu kunyakuliwa kwenye upendo wake, kwa maana hiki ni kizazi ambapo atamimina huo mto kwa wale wenye kiu, wale wapweke, kwamba atakuja na utafahamu kunyakuliwa katika upendo wake.


Mungu anapuliza tarumbeta na anawaita wale wenye sikio la kusikia. Kwa maana hiki ni kizazi ambazo anawainua watu wake wa Roho na watatembea duniani kote kama jeshi kubwa. Anashusha mifumo ya zamani iliyo waweka watu wake utumwani, na anaiharibu mifumo hiyo iliyowafanya watu wake wakose matumaini. Amechoka kusikia vilio vya watu wake, na ingawa watu wake wamekosa matumaini, atawainua na atawarejesha. Watu watalia na kutubu mbele yake na watu watamjia Yeye na kukumbatiwa na Roho wake. Watu hawatalemazwa tena na mashirika ya binadamu, yanayowaweka vifungoni, yanayowaweka mateka.


Watakwenda kama mawakala huru wa Roho Mtakatifu, nao watamtangaza kwa ujasiri jinsi alivyo. Kwa sababu watavalishwa silaha zote za kiroho, hakuna silaha inyanyukayo dhidi yao itakayofanikiwa. Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa....(Isa.54:17) Moto wa Mungu umetumwa ulimwenguni mwote kuwaleta watu wake katika utukufu, kuwalleta watu wake katika uzima tele. Usiukatae mto, bali uukaribishe moto. Kwa kweli wakati moto unapotumwa kwako,unakufanya uwe hai, unakufanya wewe uunguze, ili kwamba ukaweze kumpa Mungu sifa na kulitukuza jina lake, na kuja kwenye nuru ya utukufu wa jinsi alivyo. Wale ambao Mungu aliye Hai atawainua, watakuwa katika jeshi lake la Roho, watakuwa watu wake wa roho, jamii yake ya Roho.


Unaishi katika nyakati ambazo watu wamemwasilisha Mungu isivyo, kwa maana wamemwasilisha yeye kama mtu aliyeloweshwa maji, wamemwasilisha yeye kama kitu ambacho kinatoa moshi, na sio kiwakacho na kuunguza. Wamemwasilisha kama kipande kibichi cha kuni, kinachojaribu kuwaka, ni kitu cha kutisha walichokileta. Ni wajumbe wa uharibifu wanavyohubiri hivyo. Mungu atawatuma watumishi wake wa moto dhidi yao, nao watakwenda duniani kote kutangaza moto wake. Watawaondolea kifuniko chao cha unafiki, na watawafunua jinsi walivyo mbwa mwitu, watafunua ni watumishi wa jinsi gani walivyo. Wengi watawekwa huru kutoka katika utumwa wa giza, kutoka kwenye utumwa wa unafiki wao, kwa maana atawatuma wajumbe wake waliojaa moto.


Hakuna taasisi ya mwanadamu au muungano wa waongo utakaomsimamisha Mungu, bali atautuma moto na jeshi lake litainuka, naye atakuwa na kabila lake la kifalme lililotumwa na litamtangaza jinsi alivyo. Kuna wengine kati yenu mnaoabudu kanisa lenu na kumwabudu mchungaji wenu na ni watu wa dini sana.Mtasujudia sanamu hizo,lakini hamtamsujudia Mungu na wala hamtatafuta ushauri wake, wala kutafuta mwongozo wake kwa maana ninyi ni watu wa dini sana. Lakini kumbuka kuwa ni watu wa dini waliomwua Bwana Yesu. Msiridhike na makanisa ya kidunia, na yote hayo ambayo wangewalisha, kwa maana wanawalisha tu ili wapate pesa zenu, na wakiisha zipata pesa zenu mmebaki na kitu gani tena?


Umetiwa majeraha rohoni na viongozi vipofu na wachungaji wa uwongo. Kama utamtafuta Mungu, anao uwezo wa kukuponya majeraha yako na kukurejeshea shauku kuu uliyokuwa nayo hapo mwanzo, anao uwezo wa kukutakasa na kukufanya mpya tena na tena. Umekatishwa tamaa sana, lakini umekuwa ukitafuta miongoni mwa wafu upate uzima ambao haupo.



Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com